Tafsiri na Ukalimani

Kiini cha Tafsiri na Ukalimani hujikita katika uhawilishaji wa taarifa kutoka lugha moja kwenda lugha nyingi. Mtu anayejihusisha na masuala haya anapaswa kuwa na umilisi wa kutosha wa lugha zote mbili anazozishughulikia, kuwa na umilisi wa kutosha wa lugha moja wapo tu huweza kuzalisha kazi isiyofaa. 

Wataalamu wetu wamebobea katika matumizi ya lugha; Kiswahili, Kiingereza, Kiarabu, Kifaransa na Kichina, kwa nyanja zote kuu za lugha ikiwamo fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki. Lugha zote wamekuwa wakizishughulikia katika kazi zao za kila siku, hili limesaidia kuwajengea uwezo na uzoefu mkubwa.

Kwa wateja wetu wote wa tafsiri tunawapa huduma ya uhariri pamoja na usomaji prufu wa matini lengwa bure, uhariri na usomaji prufu baada ya kazi kutafsiriwa huleta kazi bora zaidi isiyo na makosa madogomadogo yaliyosababishwa wakati wa tafsiri. 

Wabobevu wetu wa lugha hufanya kazi zao kwa weledi mkubwa kwa njia ya kushirikiana, wasiliana nasi kwa huduma bora ya tafsiri na ukalimani wa ndani na nje ya nchi.

Tafsiri

Kwa mwezi huu wataalamu wetu wa lugha zifuatazo ratiba zao zipo wazi kukuhudumia.

Ukalimani

Kwa mwezi huu wataalamu wetu wa lugha zifuatazo ratiba zao zipo wazi kukuhudumia.

(+225) 715 001 818 | 787 001 819

info@uhariri.com