Uhariri

Uhariri wetu hubaini makosa yaliyojitokeza katika uandishi wako kwa kutumia mbinu ya usomaji wa neno kwa neno, kwa njia za kitaalamu ndani ya mfumo wa Track Changes. Lengo la uhariri ni kuondoa makosa ya uchapaji, kisintaksia, kimofolojia, kisemantiki, kiuakifishaji, mpangilio n.k

Kuna umuhimu mkubwa kwa waandishi kuwa makini wakati wa kuchagua mhariri, ni muhimu mwandishi huru kufahamu kuwa si kila mhariri anaweza kuhariri kazi yako, mhariri ambaye amejikita katika kuhariri vitabu vya watoto ni nadra kuweza kuhariri vitabu vya ujasusi na upelelezi au matangazo ya kibiashara.

Licha ya kuwa mjuzi wa lugha iliyotumika kuandika andiko, pia mhariri anapaswa kuwa na sifa nyingine za ziada, kama vile kuwa mdadisi na mtafiti wa masuala mbalimbali, kuwa ni mwenye kujifunza kila siku, kuwa mshauri nambari moja wa mwandishi, kushirikiana bega kwa bega na taasisi zinazojishughulisha na lugha kama vile BAKITA n.k.

Usisite kuwasiliana nasi ili tushirikiane kuifanya kazi yako bora (kitabu, jarida, tasnifu, tangazo, ripoti n.k) kuwa bora zaidi machoni mwa watu.

Uhariri.com

Kwa Huduma Bora Kabisa

Usalama

Kazi yako itafanywa na kuhifadhiwa kwa siri.

Muda

Kazi yako itakamilika ndani ya muda mfupi tuliokubaliana.

Gharama Nafuu

Pia tutakupa uhuru wa kulipa kwa awamu.

Wataalamu

Utahudumiwa na wataalamu wenye uzoefu wa kutosha.

Ushauri

Utakaokujenga kuwa mwandishi bora zaidi

Tutakufikia

Popote ulipo duniani. Tutakuhudumia kwa haraka.

Ushuhuda

Uhariri mnaoufanya ni wa kiwango cha juu sana, kwani humuacha mtunzi akiwa mwandishi bora zaidi kupitia ripoti zenye ushauri makini, mnazotoa kwenye kila uhariri.
Hussein Tuwa
Mwandishi wa riwaya ya Mkimbizi

(+225) 715 001 818 | 787 001 819