Mhariri Bora

Mhariri bora huwa na sifa zake, zinazompambanua na wahariri wengine. Kimekuwa ni kilio cha muda mrefu kwa waandishi wa vitabu kulalamika kuhusu mhariri au wahariri ambao hawahariri vizuri kazi zao kwa ubora walioutaraji. Wapo waliolazimika kutafuta wahariri wengine kuhariri tena miswada yao, wapo walioteketeza nakala za vitabu vilizohaririwa vibaya na kuingia hasara ya uchapishaji, wapo waliosusa na kuamua kutoa kazi zao bila kupitia kwa wahariri.
Ni ukweli uliodhahiri kuwa si kila mtu anayefahamu lugha ya Kiswahili ana uwezo wa kuhariri.  Waweza kupata mhariri bora kwa kuzingatia yafuatayo.

1. Wasiliana na wahariri.
Kama bado haujapata mhariri makini unayemwamini, wasiliana na wahariri japo watatu jenga urafiki nao kisha jadilianeni mawili matatu kuhusu uhariri wa mswada husika.

2. Omba Sampuli ya uhariri (edited sample).
Wape sehemu ndogo ya mswada wako wahariri hao kisha waombe wahariri ili uone namna wanavyoweza kubaini makosa, baada ya kupokea mrejesho wao fanya uamuzi sahihi kwa mustakabali bora wa mswada wako.

3. Fahamu muda wa kukamilika uhariri.
Si vyema mwandishi kumwachia muda mrefu sana mhariri, hii hujitokeza kwa mwandishi kuwa na matarajio kwamba muda wote huo mhariri anautumia kuboresha mswada wake. Ni vyema kufuatilia mswada wako kujua upo hatua gani ya uhariri bila kumbughudhi mhariri (usije ukakosa mwana na maji ya moto). Kufahamu zaidi kuhusu muda wa uhariri waweza bofya Muda wa uhariri.
 
4. Fahamu gharama ya uhariri.
Uhariri ni sehemu katika uandishi wa vitabu inayohitaji uwekezaji, waswahili wanasema “vya bure ghali”, usijiegemeze sana kwenye uhariri wa kishikaji ambao mshikaji anaweza akaufanya kishikaji, matokeo yake badala ya kutoa kazi nzuri unatoa kazi ya kishikaji shikaji, halafu unataraji itumike kufundishia chuo kikuu. Kufahamu zaidi kuhusu kwa nini gharama za uhariri hutofautina kutoka mhariri mmoja hadi mwingine bofya Gharama ya uhariri.
 

Hadi kufikia hapo unaweza kuchagua wapi kwa kupeleka mswada wako uhaririwe.

Uhariri.com

Kwa Huduma Bora Kabisa

Usalama

Kazi yako itafanywa na kuhifadhiwa kwa siri kubwa

Muda

Kazi yako itakamilika ndani ya muda mfupi tuliokubaliana

Gharama Nafuu

Pia tutakupa uhuru wa kulipa kwa awamu mbili hadi tatu

Wataalamu

Utahudumiwa na wataalamu wenye wabobevu wa lugha

Ushauri

Utakaokujenga kuwa mwandishi bora zaidi

Uzoefu

Tuna wataalamu wenye uzoefu wa kutosha

(+225) 715 001 818 | 787 001 819