Usanifu Kurasa
Kurasa za andiko lolote hupaswa kusanifiwa vizuri ili ziweze kufikia tija iliyokusudiwa, hili litawezekana endapo usanifu kurasa utazingatia masuala yote muhimu katika usanifu kurasa kama vile Typography, Margin, Alignment, Whitespace, Images, Widows & Orphans n.k
Kila kipengele kati ya vilivyoorodhesha hapo juu kina umuhimu wake katika usanifu kurasa wa andiko iwe kitabu, kipeperushi, tangazo, ripoti n.k, hapa tutaangalia umuhimu wa baadhi ya zipengele hivyo katika usanifu kurasa. Mosi tuanze kuangalia kuhusu Margin, hii huweka vipimo vya nafasi inayopaswa kuachwa katika pande kuu nne za kurasa yaani juu, chini, kulia na kushoto, umuhimu wa margin husaidia katika ubanaji wa vitabu (binding) kwani nafasi ya kati ikiachwa ndogo kitabu kikishabanwa maandishi ya kati yatakuwa hayasomeki.
Pili tuangalie typography (taipografia), ili andiko lisomeke kwa urahisi msanifu kurasa lazima azingatie fonts & fonts size za kila kipengele cha andiko ikiwa ni kichwa cha habari au sura, maelezo ya ndani ya andiko, namba, jina la mtunzi au mwandishi n.k. Si vyema kwa kitabu kimoja kuwa na fonts zaidi ya tatu, na kila kipengele (Sura, aya, jina n.k) vyote vinapaswa kuwa na fonts & font size za aina moja kwa kipengele husika.
Alignment, mwegamo wa maneno unapaswa kuwa sawa kuanzia kurasa wa kwanza hadi wa mwisho pia unapaswa kufanana kwa kila vipengele vinavyofanana iwe kichwa, aya, footnote, namba n.k. mwegamo wa maneno unaweza kuwa upande wa kulia, kati ama kushoto kulingana na andiko husika. Hivi ni baadhi tu ya vipengele ambavyo ni muhimu kuvizingatia katika usanifu kurasa vipo vipengele vingine lukuki ambavyo kama vyote havikuzingatiwa basi kazi yako itakuwa na mwonekano mbaya lakini pia itaongeza gharama za uchapishaji.
Usisite kuwasiliana nami ili tushirikiane kuipanga kazi yako (kitabu, jarida, tangazo, tasnifu, ripoti n.k) iwe na mwonekano bora unaovutia machoni.
Kwa nini usanifu kurasa?
Ni vyema kulipa umuhimu mkubwa suala la usanifu kurasa za andiko lako kama wanavyofanya wenzako
Hupunguza Gharama
Usanifu mzuri wa kurasa hupunguza gharama za uchapishaji, hili huwezekana kwa uteuzi mzuri wa typography & fonts size, pia kwa kuzingatia margin & nafasi baina ya aya.
Mwonekano mzuri
Mpangilio mzuri wa kurasa huifanya kazi kuwa na mwonekano mzuri unaomvutia msomaji kuisoma kazi yako mara kwa mara na kuwashawishi wengine kuisoma.
Hudhihirisha umakini
Umaniki wa mwandishi hauishii katika kuandika andiko zuri tu, bali pia huenda mbali zaidi kwa kuhakikisha anasimamia mwonekano mzuri wa kazi yaani usanifu jalada & kurasa
Mpangilio unaovutia
Kupanga ni unadhifu panga kazi yako vizuri sasa kuivutia hadhira yako. Panga pamoja nami kitabu, ripoti, jarida, kipeperushi, makala n.k. JUKUMU NI LAKO SASA USICHELEWE…